Posted by On the spot Tz
10:59:00 PM
0
Klabu ya Azam, jana Jumanne imezindua duka la vifaa vya michezo ambapo litakuwa likiuza bidhaa zenye nembo ya klabu hiyo pekee.
Miongoni mwa bidhaa ambazo zitakuwa zikipatikana katika duka hilo lililopo kwenye makutano ya mitaa ya Swahili na Mkunguni, Kariakoo jijini Dar, ni pamoja na jezi, soksi, mabegi na kofia.
Baada ya kuzindua duka hilo, Mtendaji Mkuu wa Azam, Saad Kawemba, amesema: “Huu ni mwanzo tu, tutafungua maduka mengine katika sehemu mbalimbali za jiji hili na mikoani lengo likiwa ni kuitangaza nembo yetu.”
Kawemba aliongeza kuwa, duka hilo litakuwa likifunguliwa kila siku kuanzia saa 2:30 asubuhi na kufungwa saa 2:30 usiku ambapo muda huo utatoa fursa kwa kila mmoja kwa nafasi yake kufika dukani hapo na kujipatia bidhaa za klabu yao ya Azam.
Tagged with:
MICHEZO KITAIFA.
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Makahaba Dar es Salaam Wamzidi Nguvu Paul Makonda,,,,,,,,,Ving’ang’anizi! Agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kuwataka akina dada wanaouza miili ‘makahaba’ kuondoka kwenye ‘mas...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Shilingi Bilioni 3 na Mali za Bilioni 10 zataifishwa na TRA Kutoka kwa Wakwepa Kodi Bandari Kavu ya Azam,,,,,,,Mamlaka ya kukusanya kodi TRA kupitia madalali wa Yono Auction Mart wamekusanya mali za bilioni 3 pamoja na kutaifisha mali za b...


No comments: