Posted by On the spot Tz
8:31:00 PM
0
Kikao cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 kimeendelea tena Dodoma leo April 21 2016 , shughuli nzima iliyoanza asubuhi ni maswali na majibu kwa Waziri Mkuu, Pia baadhi ya Wizara zilihusishwa katika maswali hayo, ambapo Mawaziri na Manaibu Waziri wa Wizara hizo walilazimika kuyatolea majibu.
Baadhi ya Wizara hizo ni pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambapo swali lililoulizwa na Mbunge wa Kasuru Mjini Daniel Nsanzugwanko ilikuwa ‘Je, Serikali haioni umuhimu wa kuwekeza kwakiwango kikubwa katika Mkoa wa Kigoma kwa kujenga jumba la sanaa ili vijana wawe na sehemu nzuri ya kujiendeleza kisanaa?’
Swali la pili likawa ‘Kama Serikali inakubaliana na hoja hiyo, kituo hicho kitaanza kujengwa lini?’
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akajibu ‘Wizara yangu inatambua mchango mkubwa wa wasanii wenye asili ya mkoa wa Kigoma kama vile Diamond, Alikiba, Banana, Mrisho Mpoto na wengine‘
‘Wizara yangu inaendelea kuhimiza Halmashauri na Manispaa zote nchini kutenga maeneo ya kujenga vivutio vya sanaa. Kuhusu mkoa wa Kigoma, tunashauri Serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri zote kutekeleza ujenzi wa jumba la sanaa ‘ ;-Anastazia Wambura
onthespottz.blogspot.com
Tagged with:
HABARI KITAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mwingine Adakwa Kwa Kumkashifu Rais Magufuli Kwenye Mtandao wa "WhatsApp",,,,,,,Sheria ya Makosa ya Kimtandao inaendelea kushika kasi, mwingine tena aingia matatani baada ya kubainika kutumia Lugha mbaya dhidi ya Rais ...



No comments: