Posted by On the spot Tz
10:34:00 PM
0
Chadema imetua Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kufungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu na Jeshi la Polisi ikitaka mbunge wa jImbo hilo, Godbless Lema apelekwe kortini.
Chama hicho kinaiomba Mahakama hiyo kuwaamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali na maofisa wanne wa Jeshi la Polisi akiwamo IGP, kumpeleka mahakamani mbunge huyo kwa madai amepitiliza muda wa kisheria wa kushikiliwa mahabusu na jeshi hilo.
Mbunge huyo machachari wa Chadema amekuwa rumande tangu Jumatano alipokamatwa mjini Dodoma alikokuwa akihudhuria vikao vya Bunge na kuwa kitendo cha polisi kumshikilia zaidi ya saa 24 ni kinyume cha sheria kwani amekuwa ndani zaidi ya saa 175, hivyo kinamnyima mtuhumiwa haki za kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufungua kesi hiyo, Wakili wa Chadema, John Mallya amesema leo itapangiwa jaji wa kuisikiliza na siku ya kuanza.
“Jambo ninalolifanya muda huu ni kukusanya hati za wito wa kuitwa mahakamani watu watano tuliowashitaki ambao ni Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi (Central),Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai mkoa (RCO), Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha (RPC), Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini na Mwanansheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mshauri mkuu wa kisheria na anatakiwa mahakamani kueleza kwani wanakiuka masharti ya kisheria,”amesema Mallya.
Amesema anatarajia kesi yao iliyofunguliwa chini ya hati ya dharura itasikilizwa mapema kwa sababu inahusu mtu aliyenyimwa haki ya dhamana, haki ya kutoa maelezo na haki ya kuletwa mahakamani.
“Tunataka hawa tuliowashitaki kumleta Lema mahakamani na dhamana yake ifanyiwe mchakato Mahakama Kuu na waiambie mahakama kwanini wasichukuliwa hatua za kisheria kwa kukiuka masharti ya kisheria, pia tumeomba gharama zote za hii kesi zilipwe na Serikali,” amesema Mallya.
onthespottz.blogspot.com

Tagged with:
HABARI KITAIFA
On the spot Tz
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular Posts
-
Kiongozi wa Upinzani Uganda Besigye Ashtakiwa Kwa Uhaini,,,Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye ameshtakiwa kwa kosa la uhaini baada ya kujitangaza mshindi wa uchaguzi uliofanyika hiv...
-
HARRY KANE ATWAA KIATU CHA DHAHABU ENGLAND,,,,,,,Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane akiwa na picha hya kiatu cha dhahabu cha Ligi Kuu ya Enfland baada ya kiibuka mfungaji bora...
-
Old Trafford Kwategwa Bomu Hewa,,,Mashabiki wapatao 20,000 wametolewa nje kwenye Uwanja wa Old Trafford na kusababisha kuchelewa kuanza kwa mechi katyi ya Manchester Uni...
-
Mashabiki na Wanachama wa Yanga Wachoma Magazeti Yanayomilikiwa na Reginald Mengi.,,,,,,Wanachama na mashabiki wa Yanga leo wakiyachana na kuyachoma moto magazeti ya The Guardian na Nipashe yanayomilikiwa na kampuni ya IPP MED...
No comments: