Shirika la Afya Duniani WHO latangaza kumalizika Ebola nchini Liberia,,,,,,

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza rasmi kumalizika homa ya ugonjwa hatari ya Ebola baada ya miaka miatatu ya kushuhudiwa nchini humo na kusababisha idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.
Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza rasmi leo kuwa, sasa ugonjwa huo umemalizika nchini Liberia. Ugonjwa wa Ebola ulioibuka nchini humo mwaka 2013 na kusimama mwaka jana 2015, uliibuka tena mwezi Machi mwaka huu na kusababisha mauaji ya mtu mmoja. Pamoja na hali hiyo serikali ya Monrovia haikutangaza hali ya hatari nchini humo. Baada ya hapo Shirika la Afya Duniani WHO sanjari na kutoa tahadhari kwa serikali ya nchi hiyo, lilitoa muhula wa siku 42 kwa nchi hiyo kungamiza maradhi hayo, ambao unamalizika leo Alkhamis Juni Tisa. Katika kipindi hicho hakuna kesi yoyote iliyoripotiwa kuhisiana na ugojwa huo. Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani kuanzia mwezi Disemba mwaka 2013, karibu watu elfu 26 waliripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo hatari huku wengine elfu 11 wakipoteza maisha.
onthespottz.blogspot.com
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply