Rais Barack Obama wa Marekani ametangaza kuwa serikali ya Washington karibuni hivi itatuma askari 250 wa nchi kavu kwenda Syria kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi.
Akiongea mjini Hannover nchini Ujerumani hapo jana, Rais Obama alisema Washington katika kipindi cha wiki kadhaa zijazo itatuma askari 250 zaidi kuungana na Vikosi vya Operesheni Maalumu vya Marekani ili kuungana na vikosi vya nchi hiyo eti kukabiliana na kundi la kigaidi la ISIL.
Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita, rais huyo wa Marekani alipuuzilia mbali wazo la kutumwa vikosi zaidi vya kigeni katika nchi hiyo ya Kiarabu.
Kutumwa askari hao kutapelekea idadi ya askari wa Marekani walioko nchini Syria kufika 300.
Hii ni licha ya Muhammad Jihad al-Laham, Spika wa Bunge la Syria hivi karibuni katika mazungumzo yake na ujumbe kutoka Ulaya kusema kuwa, vita dhidi ya ugaidi iwe ni nchini Syria, Ulaya au katika nchi nyingine ni jambo ambalo linahitajia ushirikiano ili ulimwengu uweze kuliondoa donda hili la saratani na kusisitiza kuwa, kuna nchi nyingi duniani hususan Marekani, Saudia, Qatar, Uturuki na nyinginezo ambazo zinatoa himaya kwa magaidi.
Karibu watu laki 5 wameuawa tangu Machi mwaka 2011, baada ya Marekani na waitifaki wake katika eneo hili kuivamia Syria kwa kisingizio cha kupambana na kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply