Hassan  Kessy

Beki mpya wa Yanga, Hassan Kessy amesema kati ya vitu anavyo vitamani baada ya kutua kwenye timu hiyo, basi ni kuwepo kwenye kikosi kitakachoivaa TP Mazembe ya DR Congo.

Yanga inatarajiwa kuvaana na Mazembe kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika wakiwa Kundi A. Timu nyingine za kundi hilo ni MO Bejaia ya Algeria na Medeama ya Ghana.

Kundi B lina timu za Kawkab na FUS Rabat zote za Morocco, Etoile du Sahel (Tunisia) na Ahly Tripoli ya Libya.  

Kessy amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga kwa dau la Sh milioni 40, huku akilipwa mshahara wa Sh milioni mbili akitokea Simba kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.

Kessy alisema kikubwa anachotaka ni kutengeneza rekodi ya kucheza na moja ya klabu kubwa Afrika ambayo ni Mazembe anayoichezea Mtanzania Thomas Ulimwengu.

Kessy alisema, anaamini kama akicheza mechi hiyo ya Mazembe, huo ndiyo utakuwa mwanzo mzuri wa yeye kujitengenezea soko kwa kuonyesha kiwango kikubwa.

Alisema akiwa anaichezea Simba hakuipata nafasi hiyo, hivyo anaamini huo ndiyo mwanzo mzuri kwa yeye kujitangaza kimataifa kupitia michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wanayoshiriki Yanga.

“Mechi ya Mazembe ninaitamani sana kuliko vitu vyote, naamini nikicheza mechi hiyo nitajitengenezea nafasi nzuri ya mimi kujitangaza kimataifa hii itakuwa rekodi kwangu.

“Muda mrefu nikiwa ninaichezea Simba, nilikuwa natamani kucheza michuano ya kimataifa ambayo sikupata nafasi hiyo.


“Lakini hivi sasa nipo na Yanga, huu ndiyo wakati wangu muafaka wa kujitangaza kimataifa,” alisema Kessy.

SOURCE; CHAMPIONI.
«
Next

Newer Post

»
Previous

Older Post


No comments:

Leave a Reply